Psalms 77:16-19


16 aMaji yalikuona, Ee Mungu,
maji yalikuona yakakimbia,
vilindi vilitetemeka.

17 bMawingu yalimwaga maji,
mbingu zikatoa ngurumo kwa radi,
mishale yako ikametameta huku na huko.

18 cNgurumo yako ilisikika katika upepo wa kisulisuli,
umeme wako wa radi ukaangaza dunia,
nchi ikatetemeka na kutikisika.

19 dNjia yako ilipita baharini,
mapito yako kwenye maji makuu,
ingawa nyayo zako hazikuonekana.

Copyright information for SwhKC